Idara Mbalimbali

KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI

Idara ya Rasilimali Watu

Mpango ya Idara ni mpya imeanza mwanzoni mwa mwaka 2018. Wajibu wake mkubwa ni kusimamia na kurasimisha taarifa za wafanyakazi wa Taasisi za DKAK pamoja na kuandaa mpango wa kudhibiti raslimali watu na kupunguza migogoro katika sehemu za kazi. Kuandaa será ya utumishi na kusimamia haki za watumishi kwa mujibu wa kanuni za kazi za Dayosisi.

Idara ya Miradi na Mali

CORRIDOR SPRINGS HOTEL

Arusha Lutheran Medical Center

Nyumba Za Mikopo

Nyumba Za Wamama Wajane

Mradi wa Maji

Utangulizi

Idara ya Miradi   na  mali  inahusika na usimamizi wa Miradi ya huduma kwa jamii na   ya uchumi.Miradi ya jamii ni ile miradi inayohusika katika kuboresha hali ya maisha ya jamii.

Miradi ya Uchumi  ni vitega uchumi kwa ngazi mbalimbali katka dayosisi. Lengo la miradi yote ni kutekeleza utume wa dayosisi yetu ambao ni KUMHUDUMIA MTU KIROHO, KIMWILI NA KIAKILI.

Idara hii ni moja kati ya Idara tano zilizoko chini ya Halmashauri ya Mipango, Fedha na Utawala  katika Dayosisi ya Kaskazini Kati. Idara hii inashughulika ma masuala yafuatayo:-

  1. Kushirikiana na majimbo, sharika na Taasisi mbalimbali za Dayosisi kubuni, na kutekeleza miradi ya Uchumi na Huduma za jamii katika maeneo yao.
  2. Kusimamia na kutolea taarifa miradi ya kazi za umoja wa Kanisa zinazotekelezwa na Dayosisi.
  3. Kutoa taarifa ya miradi inayofadhiliwa kutoka ndani na nje ya nchi.
  4. Kuandaa mfumo mzuri wa ushirikishwaji wa wadau katika uibuaji na uendelezaji wa miradi.
  5. Kuandaa Sera kulingana na hitaji.

Miradi ya uchumi

Kwa wakati huu Dayosisi ina Hotel ya Arusha Corridor Springs kama mradi wa kiuchumi pamoja na Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre. Kituo chetu cha Mikutano cha Oldonyosambu kwa ajili ya mikutano semina, Maburudisho nk.Iko katika miteremko ya Mlima Meru upande wa Kaskazini Mashariki barabara iendayo Namanga-Kenya.

MIRADI YA JAMII

Dayosisi imewajengea wamama walezi pekee/wajane nyumba zaidi ya 145 kwa mkopo wa bei nafuu na bado inaendelea kujenga nyumba kumi kwa walengwa kama hao kutokana na marejesho ya mkopo wa nyumba hizo.

Idara ya Elimu

Utangulizi

Dayosisi ya Kaskazini Kati ina taasisi za elimu ambazo zimegawanyika katika mkundi makuu matatu.

Shule za msingi

Shule za msingi 3 zinazoanza na madarasa ya awali ambazo ni Kimandolu, Ilboru na Tetra (Enkarenarok)

Shule za sekondari

Shule za sekondari 8 ambazo ni Kimandolu,Tetra, Ngateu, Ekenywa, Enaboishu, Peace House sekondari, Moringe na Sekondari ya wasichana wa Maasae.

Vyuo vya Ufundi

Vyuo vya Ufundi 2 ambazo ni Chuo cha Kilimo, mifugo na Ufundi-BACHO na Chuo cha ufundi kilichoko Olokii.

Shule hizi zilianzishwa kwa nyakati tofauti zikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi ambao walihitaji kupata elimu ya sekondari lakini wakaikosa kutokana na  kuwa na shule chache kwa wakati huo zilizomilikiwa na serikali. Baadhi ya shule hizi zilianzishwa na wakristo/sharika kwa kuchangisha michango na nyingine  zilianzishwa kwa ushirikiano na wafadhili.

Kila taasisi ina Maono na Utume wake katika kufikia malengo yake ambayo imelenga kwenye Maono na utume wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Takwimu katika idara ya elimu

Shule za msingi kuna jumla ya waalimu 57 na watumishi wasio waalimu 21. Shule za sekondari kuna jumla ya waalimu 147 na watumishi wasio waalimu 122. Shule za sekondari kuna jumla ya waalimu 13 na watumishi wasio waalimu 12.

PEACE HOUSE SECONDARY SCHOOL

ENABOISHU SECONDARY SCHOOL

Idara ya Afya

Utangulizi

“Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, Asema BWANA” Yeremia 30:17a.

Idara ya Afya inazidi kumshukuru Mungu kwa kuwezesha vitengo vyake mbali mbali kutekeleza vyema shughuli zake kwa kipindi cha mwezi Januari  hadi Machi 2018.

Mpaka kufikia tarehe  ya taarifa hii…

  1. Idara ya Afya ina Zahanati 7 zinazofanya kazi.
  2. Kituo cha Afya 1.
  3. Hospitali 3.
  4. Taasisi 2 za kutolea mafunzo  (Training Institutions ) ambazo ni ALMC Surgery Residency programme na ALMC Nursing school.

Sambamba na vituo tajwa hapo juu, Idara inayo Miradi mbali mbali kama vile Mradi wa kuzuia na kupambana na Ukimwi (USAID Boresha Afya), Huduma ya Faraja na Tiba Shufaa (Hospice & Palliative Care service), Mradi wa Fistula, mradi wa kutunzia wagonjwa waliorekebishwa mifupa kwa njia ya upasuaji (Plastic surgery) na Mradi wa kuzuia na kudhibiti magonjwa ya macho (Eye Mobile Clinic).

Idadi ya watumishi katika vituo vyetu ni 732.  Mchanganuo wa watumishi hao kutokana na kada zao ni kama ifuatavyo:-

  1. Madaktari  71.
  2. Wauguzi  208.
  3. Wengineo 453.

Arusha Lutheran Medical Center

Selian Lutheran Hospital

Kirurumo Health Center

Idara ya Hazina

Utangulizi

Wajibu wa Idara ni kusimamia mapato na matumizi ya Dayosisi na kuratibu mali zote za Dayosisi. wajibu wa Idara ya Hazina ni:-

  1. Kuhakikisha Mapato yanapatikana kwa Wakati
  2. Kufunga Hesabu za kila Mwaka
  3. Kufanya Ziara Katika Taasisi , Majimbo na sharika za Dayosisi kwa ajili ya kuelekeza
  4. Kutoa semina za utendaji wa kazi kwa watunza hazina ngazi za Majimbo na Sharika.

IDARA YA HAZINA

KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI