MISSIONI NA UINJILISTI

KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI

KANISA LA KILUTHERI LA ILBORU LA ZAMANI

KANISA LA KILUTHERI LA ILBORU LIPYA

Utangulizi

Halmashauri ya Misioni na Uinjilisti inashughulikia mambo ya Misioni na Uinjilisti na Jinsia.  Halmashauri hii ndiyo inayoshughulikia na kutunza mambo yote yanayohusu mfundisho na Maadili.

Halmashauri ya Misioni na Uinjilisti ina idara mbili:-

 1. Idara ya Misioni na Uinjilisti
 2. Idara ya Jinsia

Idara ya Misioni na Uinjilisti

Idara ya Misioni na Uinjilisti inashughulikia mambo yote ya Misioni, Uinjilisti, Uwakili na mambo yote ya Kiroho. Lengo la Idara hii ni kuendeleza Agizo kuu la Utume la Bwana wetu Yesu Kristo kama lilivyo katika Mathayo 28: 19-20.
Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama mimi nipo pamoja nayi siku zote hata ukamilifu wa dahari.

Kazi za Idara ya Misioni na Uinjilisti

 1. Kuandaa sera ya Misioni na Uinjilisti itakayotumika katika ngazi zote za dayosisi
 2. Kuweka mikakati kati ya Wachungaji, Wainjilisti na Wakristo wote katika kutekeleza agizo la Bwana wetu Yesu Kristo
 3. Kuandaa na kuratibu mikutano mikubwa ya Kiroho ya Ki-Dayosisi, semina na warsha mbalimbali
 4. Kuhakikisha kuwa ibada, Mikutano ya Kiroho na semina zinazofanyika katika sharika za dayosisi zinafuata ta kanisa letu (KKKT)
 5. Kusimamia, kuratibu na kutoa taarifa za vitengo vyote vilivyopo chini ya idara hii na kuwasilisha taarifa hizo kwenye Halmashauri ya Misioni na Uinjilisti

Vitengo vya Idara ya Misioni na Uinjilisti

 1. Elimu ya Kikristo na Wanafunzi
 2. Mafunzo ya Theologia kwa njia ya Enezi
 3. Muziki na Uimbaji
 4. Udiakonia
 5. Uamsho

Mafunzo ya Theologia kwa njia enezi

Ni kitengo kinachotoa mafunzo mbalimbali ya Theologia kwa Wainjilisti na mafunzo mengine kwa wanadayosisi.

Kazi za kitengo cha Mafunzo ya Theologia kwa njia enezi

 1. Kuandaa wainjilisti kwa cheti kinachokubalika na Dayosisi na Kanisa.
 2. Kubuni na kuanzisha mafunzo ya aina mbalimbali yanayoilenga jamii kwa manufaa ya kazi ya Injili.
 3. Kuwatembelea wanafunzi katika vituo na kuwafundisha kwa utaratibu uliowekwa na bodi.

Elimu ya Kikristo

Kitengo hiki kinashughulikia mambo yote ya mafundisho ya dini katika shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Kipaimara na Ubatizo.

Kazi za Kitengo cha Elimu ya Kikristo

 1. Kusimamia na kuelekeza ufundishaji na Malezi kwa neno la Mungu katika shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Kipaimara na Ubatizo kwa kufuata utaratibu wa Kanisa letu (KKKT) na Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT).
 2. Kuhakikisha kuwepo mitaala inayotolewa na Kanisa (KKKT), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na walimu walioandaliwa vyema katika fani hiyo.

Muziki na Uimbaji

Kitengo hiki kinashughulikia mambo yote yahusuyo Kwaya,  muziki, uimbaji na uenezaji wa taaluma ya muziki na uimbaji     katika Dayosisi.

Kazi za Kitengo cha Uimbaji

 1. Kufundisha kwa usahihi uimbaji na muziki kwa kufuata misingi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri.
 2. Kufundisha muziki katika Majimbo na Sharika zetu zote na kuweka mkazo wa uimbaji bora wa Litrugia ya Kanisa letu.
 3. Kufuatilia, kushauri na kuratibu uimbaji katika Majimbo na Sharika.
 4. Kwaya zioneshe uchaji na nidhamu wakati wakumwimbia Mungu wawapo mahali popote, kwa maneno, matendo na mavazi yao.
 5. Kwaya zisiimbe ibadani kwa kutumia CD, VCD, DVD, VHS, Flash, memory au Audio.
 6. Kwaya zisiende popote ndani au nje ya Usharika wala kuchangisha fedha bila idhini ya Mchungaji Kiongozi.
 7. Kazi zote za sauti na video za vikundi vyote vya kwaya ndani ya Dayosisi vitasajiliwa na kulindwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamsho

Huu ni mpango wa dayosisi wa kuamsha wakristo kiroho kwa njia ya Neno la Mungu, Mikutano, Semina, Makongamano na maombi.  Mkristo anapata tena nguvu na maisha mapya na kujitambua baada ya kujitathimini katika maisha na mwenendo wa kikristo.

Kazi ya Kitengo cha Uamsho

Kuamsha na kulea wakristo kiroho kwa njia ya Neno la Mungu, Mikutano, Semina, Makongamano na maombi.

Udiakonia

Hii ni huduma katikati ya wahitaji na msingi wake ni kwenye neno la Mungu. (1Timotheo 5:1-3)

Kazi za Kitengo cha Udiakonia

 1. Kuandaa na kusimamia Sera na Miongozo ya Udiakonia kwa mujibu wa taratibu za Dayosisi yetu.
 2. Kusaidia makundi maalum kama yatima wajane na wazee
 3. Kutoa semina za kuhudumia wahitaji
 4. Kutambua wahitaji na kuwasaidia
 5. Kuwawezesha wahitaji kuweza kujitegemea wenyewe

Huduma ya Yatima na wajane Mwika (HUYAMWI).

Mtoto Yatima Maana yake nini.

Yatima ni watoto  wasiokuwa aidha na mzazi moja au wazazi wote. Kuna wengine  wasiokuwa  hata na jamaa wa karibu. Wote hawapo.

Yatima hao walipatikana kwa sababu ya vifo vya wazazi wao vilivyotokana na ajali za kushambuliwa na wanyama wakali, vita vya wenyewe kwa wenyewe na magonjwa yaliyokosa tiba  kama UKIMWI.

Huduma hii imeanza katika Dayosisi katika sharika sita za majaribio na mwaka 2017 ziliongezeka sharika zingine tano. Kwa hiyo huduma hii inaendelea vizuri. Tunapenda kutoa wito kwa sharika zote za Dayosisi kuwatambua yatima na wajane katika sharika zao, maana tukiwajua hao na kuwahudumia ndipo Mungu atakapotubariki zaidi.

Nyumba Ya Mama Mjane na Familia yake

Wanawake, Wanaume, Vijana na Watoto.

Ijue Idara ya Jinsia

Utangulizi

Idara hii inashughulikia maendeleo na mambo yote yanayohusu Wanawake,Wanaume,Vijana na Watoto. Kutokana na changamoto zilizopo kati ya Watoto,Vijana,Wanaume na Wanawake Idara itajikita katika kuhusisha vitengo vyote ili kuhakikisha jamii yote inaguswa na kushirikiana katika kupunguza na kuleta maendeleo Endelevu ndani na nje ya Dayosisi.

Kutokana na mgawanyiko wa majukumu ya Kijinsia Idara in vitengo vinne ndani yake ili kusaidia kufikia malengo tajwa hapo juu. Pia ili kufikisha kwa kiasi huduma  na kurahisiha utekelezaji wa kazi kwa kila mhitaji Idara ina husika moja kwa moja na vitengo vyote kwaajili ya ufanisi wa malengo tarajiwa.

Baadhi ya majukumu ya Idara ya Jinsia

 1. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu wanawake, wanaume, vijana na watoto.
 2. Kuratibu maombi kwa ajili ya kanisa na familia.
 3. Kuandaa mikutano, semina, warsha na makongamano kwa wanawake na wanaume ili kupata maendeleo shirikishi na endelevu.
 4. Kuhakikisha haki za wanawake, wanaume, vijana na watoto hazikiukwi na uwakilishi wa jinsi zote katika vikao unazingatiwa.
 5. Kutoa mafundisho na elimu kwa jamii dhidi ya ndoa, mila potofu, kazi za mikono na uwajibikaji kwenye familia unazingatiwa.
 6. Kuhakikisha na kuwahimiza wanaume kutimiza wajibu wao wa kufanya kazi na kutunza familia kwa kufuata maagizo ya Neno la Mungu.
 7. Kupokea , kuandaa na kuweka utaratibu wa maombi ya Dunia kuanzia ngazi ya Sharika.

IDARA YA JINSIA

Kitengo cha Wanawake

Utangulizi

Kitengo cha wanawake kilianza mwaka 1973 wakati Dayosisi ya Kaskazini Kati ilipoanzishwa kutokea Dayosisi ya Kaskazini Moshi, wakati huo ikiitwa “Umoja Wa wa Wanawake Wakristo” (UWW) Sinodi Mkoani Arusha.

Wanawake ni kundi kubwa katika kanisa kwani ni zaidi ya asilimia 50 ya washiriki wote katika kanisa. Pamoja na mchango wao mkubwa katika kanisa, wanawake hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na mfumo dume  uliojengeka kwenye jamii kutokana na mila potofu. Mawazo potofu ya jamii kuwa “mahali pa mwanamke ni jikoni au nyumbani” ni changamoto nyingine ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya wanawake. Kitengo cha Wanawake inaendelea na jitihada za kuwahamasisha na kuwaelimisha wanawake na jamii ili kuondokana na mawazo haya pamoja na fikra potofu ambazo zinachangia katika kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo Jamii na Kanisa kuhusu umuhimu wa wanawake katika maendeleo ya Jamii na Kanisa kwa ujumla.

Malengo makuu ya Kitengo cha Wanawake

Shughuli za Kitengo cha Wanawake zimejikita katika kuwajengea wanawake uwezo wa kiimani ambapo msingi wake ni Neno la Mungu. Wanawake pia wanajengewa uwezo wa uongozi pamoja na uwezo wa kuanzisha na kusimamia shughuli za ujasiriamali kwa lengo la kuongeza kipato na kupunguza umaskini.

Majukumu ya Kitengo cha Wanawake

Kuandaa ,kuratibu na kufundisha semina mbalimbali ili kuwajengea wanawake uwezo pamoja na kuwawezesha kupata ujuzi na maarifa katika nyanja mbalimbali. 

 1. Kutoa elimu ya Masomo ya BIBLIA, kufanya uinjilisti  pamoja na MAOMBI
 2. Kuhakikisha haki za wanawake hazikiukwi na uwakilishi wa wanawake katika vikao vyote unazingatiwa.
 3. Wanawake wa Biblia.
 4. Ujasiriamali; Kitengo cha wanawake kinaandaa na kufundisha ujasiriamali pamoja na kuratibu maonesho ya kazi za mikono ya wanawake.
 5. Kilimo cha mazao mbalimbali pamoja na bustani ya mbogamboga na miti ya matunda.
 6. Utunzaji wa mazingira; Wanawake wanajifunza pia juu ya utunzaji wa   mazingira kwa kushirikiana na wadau wengine ili kukabiliana na wimbi la mabadiliko ya tabia ya nchi.
 7. Ufugaji wa kuku, mbuzi wa maziwa, na ng’ombe wa maziwa.
 8. Lishe bora kwa watoto, wanawake, wazee’ wagonjwa na jamii. Suala la lishe ni pamoja na kuzingatia umuhimu wa ulaji wa vyakula vya kiasili.
 9. Utunzaji na malezi bora ya watoto kwa kuzingatia Neno la Mungu. “Mlee mtoto katika njia ifaayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee” Mithali 22:6.
 10. Afya ya wanawake kuhamishi upimaji, kujitunza na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na HIV/AIDS, na Saratani ya shingo ya uzazi.

IDARA YA JINSIA

Kitengo cha Wanaume

Utangulizi

Kitengo hiki kinashughulikia maendeleo na mambo yote yanayohusu wanaume katika Dayosisi

Kazi za Kitengo cha Wanaume

 1. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu wanaume katika sharika zote ndani ya Dayosisi
 2. Kuomba kwa ajili ya kanisa na familia.
 3. Ulinzi na utunzaji wa familia
 4. Kuibua na kuendeleza vipawa mbalimbali walivyonavyo wanaume na kuwawezesha kuvitumia vyema katika kuendeleza Familia, Kanisa na Taifa kwa ujumla
 5. Kuimarisha na kuendeleza kazi za injili kuanzia ngazi ya familia
 6. Kupinga mila potofu zinazoathiri wanaume na wanawake kiroho, kisaikolojia, kijamii na kimwili

IDARA YA JINSIA

Kitengo cha Vijana

Madhumuni ya Kitengo cha Vijana

 1. Kuwasaidia vijana wampokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
 2. Kuwalea vijana kimwili, kiakili na kiroho katks sharika kwa njia zifuatazo
  • Ibada
  • Semina za Neno la Mungu
  • Makangamano na midahalo ya Neno la Mungu
  • Kuwashrikisha vijana kazi za misioni ndani na nje ya kanisa
  • Kuboresha maisha ya vijana kwa kuwapatia
   • Semina ya ujasiriamali na kuwawezesha kuanzisha miradi midogo ya uzalishaji mali
   • Kuwapa semina ya utamaduni, siasa na elimu ya afya
   • Kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kanisa, maendeleo binafsi, maendeleo ya jamii na Taifa
 3. Kuwajengea uwezo wa kutatatu matatizo yao

Mipango ya Kitengo cha Vijana

 1. Kuhamasisha sharika, taasisi/idara mbalimbali, vyama vya hiari kuhusu sera ya vija KKKT/Dayosisi ya Kaskazini Kati
 2. Kuwainua vijana kiroho iiwawe wakristo wema wanaomkiri na kumwamini Bwana Yesu
 3. Kukusanya takwimu za vijana, shuhghuli zao na kuanzisha mfumo wa kubadilishana taarifa
 4. Kuwasaidia vijana kujiimarisha katika ajira isiyo rasmi
 5. Kuimarisha michezo mbalimbali (utamaduni) miongoni mwa vijana ili kukuza vipawa vya ubunifu

Tamasha la Vijana

IDARA YA JINSIA

Kitengo cha Watoto

Utangulizi

Methali 22:6

Maono: Watu wenye furaha ,amani na          Tumaini la  kuurithi uzima wa milele kupitia Yesu Kristo.

Motto: Malezi na Maadili mema

Dira yetu: Kuwafikia watoto wote kwa injili , Elimu na Malezi

Dhima ya idara: Kusimamia  uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya mtoto kikamilifu

MALENGO

 • Kumfikia kila mtoto kwa neno la Mungu katika ukweli na usafi wote 1tim 4:12
 • Kuwalea na kuwaimarisha katika maisha ya ufanisi
 • Kutoa mwongozo katika maisha ya mtoto na jamii yake
 • Kutoa Elimu ya kiroho za kawaida kwa watoto
 • Kuwaelekeza watoto wawe wanafunzi wakati wote wa maisha yao waweze kujitegemea na kutegemewa
 • Waunganishe ujuzi wa Neno la Mungu na Elimu ya kawaida Meth: 4:10
 • Kuwalea katika mfumo unaojali kufikiria na kusaidia wengine
 • Kuwasaidia kuboresha maisha kwa kubuni miradi midogomidogo

VITENGO

Shule ya Jumapili

Hiki ni kitengo cha msingi katika kanisa        ambacho watoto wanaandaliwa ibada takatifu wakifundishwa na walimu wenye semina za walimu picha za watoto na walimu.

Shule za Awali kindagatern

Shule hizi zinafundisha kufuata muhtasari ya serikali na kanisa lengo ni kuwaimarisha        watoto katika imani yao.

 

Compassion

Nisharika linalosaidia watoto masikini wa           masikini na washirika wenza. Hivyo tuna vituo vya huduma ya mtoto  17 katika Dayosisi .

Yatima na Maskini

Sharika zetu zinatoa huduma maalum kwa watoto wahitaji na yatima huduma hizo ni Upendo Elimu na Ushauri kwa wenzio na baba na mama.