KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI
'Karibu tovuti ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati. Dayosisi yetu inashughulika na idara mbalimbali za maendeleo ya kiroho na kijamii.'
Kuhusu SisiMAONO YA DAYOSISI YA KASKAZINI KATI
“Watu wenye furaha, amani na tumaini la kuurith uzima wa milele kupitia Yesu Kristo.”
KUHUSU SISIUTUME WA DAYOSISI YA KASKAZINI KATI
Kumhudumia mtu kikamilifu Kiroho, Kiakili na Kimwili
KUHUSU SISI
Neno La Utangulizi Kutoka Kwa Askofu
KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Kati, inamshukuru Mungu kwamba katika hekima yake isiyopimika, na kwa njia ya Mwana wake Yesu Kristo, ametuunganisha waumini wake wote ulimwenguni kuwa wamoja.
Kwa njia hiyo, tunaweza kushirikiana pamoja na kufanikishwa katika mambo mengi. Dayosisi yetu inajihusisha na huduma mbalimbali za kijamii, kiroho, kiuchumi na kiakili kupitia idara za Misioni na Uinjilisti, Jinsia, Diakonia, Ibada na Muziki, Afya, Elimu, Mipango, Fedha na Utawala. Dayosisi ina Majimbo Saba Kanisa Kuu na Sharika 137.
Tovuti hii kwa namna iliyo bora, inaeleza mambo yote yanayofanywa na Dayosisi hii pamoja na Uongozi wake. Tunakukaribisha kutembelea Tovuti yetu.
“Tazama jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja”. Zab 133:1.
Wenu,
Askofu Dkt. Godson Abel Mollel
Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati.
KUHUSU SISI
Dayosisiya Kaskazini kati ya KKKT ilianza mwaka 1973, wakati huo ikijulikana kwa jina la Sinodi Mkoani Arusha, iliyoongozwa na Mchungaji Mesiaki Kilevo; akiwa kiongozi wa kwanza wa Sinodi ikiwa na Washarika 30,000, Sharika 20 na Mitaa 110.
Kiongozi wa Pili wa Sinodi alikuwa hayati Askofu Dkt Thomas Olmorijoi Laiser kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1986.
Mwaka huo wa 1986 Sinodi ilibadilika kuwa Dayosisi Mkoani Arusha na Askofu wa kwanza akawa hayati Askofu Dkt Thomas Olmorijoi Laiser.
Mwaka 2010 Dayosisi Mkoani Arusha ilibadili jina na kuwa Dayosisi ya Kaskazini Kati, baada ya Serikali ya awamu ya tatu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuamua kuugawa Mkoa wa Arusha na kutokeza mikoa ya Arusha na Manyara.
Idara ya Miradi na Mali
Utangulizi
Idara ya Miradi na mali inahusika na usimamizi wa Miradi ya huduma kwa jamii na ya uchumi.Miradi ya jamii ni ile miradi inayohusika katika kuboresha hali ya maisha ya jamii.
Miradi ya uchumi
Kwa wakati huu Dayosisi ina Hotel ya Arusha Corridor Springs kama mradi wa kiuchumi pamoja na Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre.
MIRADI YA JAMII
Dayosisi imewajengea wamama walezi pekee/wajane nyumba zaidi ya 145 kwa mkopo wa bei nafuu na bado inaendelea kujenga...
Idara ya Elimu
Utangulizi
Dayosisi ya Kaskazini Kati ina taasisi za elimu ambazo zimegawanyika katika mkundi makuu matatu.
Shule za msingi
Shule za msingi 3 zinazoanza na madarasa ya awali ambazo ni Kimandolu, Ilboru na Tetra (Enkarenarok)
Shule za sekondari
Shule za sekondari 8 ambazo ni Kimandolu,Tetra, Ngateu, Ekenywa, Enaboishu, Peace House sekondari, Moringe na Sekondari ya wasichana wa Maasae.
Vyuo vya Ufundi
Vyuo vya Ufundi 2 ambazo ni Chuo cha Kilimo, mifugo na Ufundi-BACHO na Chuo cha ufundi kilichoko Olokii.
Ijue Idara Ya Jinsia Katika Dayosisi ya kaskazini Kati
Idara hii inashughulikia maendeleo na mambo yote yanayohusu Wanawake,Wanaume,Vijana na Watoto.
Menejimenti ya Dayosisi
Wasiliana Nasi
- Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
- Dayosisi ya Kaskazini Kati
- Simu: +255 272 508 039
- E-Mail:info@elctncd.or.tz
- P.O. Box 519, Arusha, Tanzania