Idara Mbalimbali

KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI

Idara ya Rasilimali Watu

Idara ya hii inayoshughulikia masuala yanayohusu watumishi wa Dayosisi. Tunaamini kuwa watumishi ni rasilimali muhimu zaidi katika kufanikisha malengo ya Dayosisi yetu. Idara ya Rasilimali Watu inajikita katika kuajiri, kulea, kuboresha, na kuhifadhi vipaji bora vinavyoiwezesha Dayosisi yetu kutoa huduma bora kwa jamii. Miongoni mwa majukumu ya Idara ni pamoja na;

  • Kuandaa na kusimamia Sera za utunzaji wa utumishi
  • Kuratibu taratibu zote za ajira, tathmini ya utendaji, kupandishwa au kushushwa cheo kwa watumishi, ustawi wa wafanyakazi, motisha, mahitaji ya mafunzo, usitishaji wa ajira na nidhamu.
  • Kuhakikisha kuwa kuna uhusiano mzuri katika eneo la kazi na kwamba migogoro yote inatatuliwa kwa wakati kulingana na taratibu za Dayosisi na Sheria za nchi.
  • Kuratibu mchakato wa ajira na uajiri wa wafanyakazi wapya.
  • Kukuza maendeleo ya kitaaluma kwa wafanyakazi kupitia mafunzo na warsha.
  • Kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi na mazingira bora ya kazi.

Dira Yetu:

Kuwa Idara inayoongoza kwa ufanisi, uwajibikaji, na ubunifu katika usimamizi wa rasilimali watu, kwa kuimarisha ustawi na maendeleo ya wafanyakazi kwa ajili ya mafanikio ya taasisi.

Dhima Yetu:

Kutoa huduma bora za rasilimali watu kwa kutumia mifumo ya kisasa, sera bora, na usimamizi wa haki, ili kujenga mazingira ya kazi yenye motisha, heshima, na ufanisi.

Idara ya Miradi na Mali

CORRIDOR SPRINGS HOTEL

Arusha Lutheran Medical Center

Nyumba Za Mikopo

Nyumba Za Wamama Wajane

Mradi wa Maji

Utangulizi

Idara ya Miradi na Malini moja kati ya Idara tano zilizoko chini ya Halmashauri ya Mipango, Fedha na Utawala katika Dayosisi ya Kaskazini Kati. Idara hii inayohusika kuratibu, kusimamia, na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi, na Huduma.

Miradi ya Kiuchumi

  1. Hoteli
  2. Hostel
  3. Nyumba
  4. Kumbi za mikutano

Miradi ya huduma

  1. Hospitali
  2. Zahanati
  3. Vituo vya Afya
  4. Shule

Miradi ya jamii

  1. Ufugaji nyuki na Mazingira
  2. Nyumba za Mafundi na Walezi pekee/Wajane

Miradi ya Uchumi  ni vitega uchumi kwa ngazi mbalimbali katka dayosisi. Lengo la miradi yote ni kutekeleza utume wa dayosisi yetu ambao ni KUMHUDUMIA MTU KIROHO, KIMWILI NA KIAKILI.

Idara hii inashughulika na masuala yafuatayo:-

  1. Kushirikiana na majimbo, sharika na Taasisi mbalimbali za Dayosisi kubuni, na kutekeleza miradi ya Uchumi na Huduma za jamii katika maeneo yao.
  2. Kusimamia na kutolea taarifa miradi ya kazi za umoja wa Kanisa zinazotekelezwa na Dayosisi.
  • Kutoa taarifa ya miradi inayofadhiliwa kutoka ndani na nje ya nchi.
  1. Kuandaa mfumo mzuri wa ushirikishwaji wa wadau katika uibuaji na uendelezaji wa miradi.
  2. Kuandaa Sera kulingana na hitaji.

Idara ya Elimu

Utangulizi

Idara hii ni mhimili muhimu katika usimamizi, uratibu, na uendelezaji wa huduma za elimu ndani ya Dayosisi yetu. Idara imejikita katika kutoa elimu bora, jumuishi, na yenye misingi ya kiroho kwa watoto, vijana, na watu wazima, kwa lengo la kuijenga jamii yenye maarifa, maadili na matumaini.

Dayosisi ya Kaskazini Kati ina taasisi za elimu ambazo zimegawanyika katika mkundi makuu matatu.

Shule za msingi

Dayosisi ina shule za msingi (3) zinazoanza na madarasa ya awali hadi darasa la saba. Shule hizi ni shule ya Kimandolu, Ilboru na Tetra (Enkarenarok)

Shule za sekondari

Dayosisi ina shule za sekondari (6) ambazo ni Kimandolu, Ngateu, Enaboishu, Peace House, Moringe na Sekondari ya wasichana wa Maasae.

Vyuo vya Kati

Diyosisi ina chuo cha Teknolojia, Ujasiriamali na Ushirika Monduli (MITEC) na Chuo cha ufundi kilichoko Olokii.

Kila taasisi ina Maono na Utume wake katika kufikia malengo yake ambayo imelenga kwenye Maono na utume wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.

PEACE HOUSE SECONDARY SCHOOL

ENABOISHU SECONDARY SCHOOL

Idara ya Afya

Utangulizi

Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, Asema BWANA” Yeremia 30:17a.

Tukiwa sehemu ya mwili wa Kristo unaohudumia jamii kwa upendo, Idara ya Afya ya Dayosisi imejikita katika utoaji wa huduma bora za afya zenye huruma, utu na ufanisi kwa watu wote bila ubaguzi, kwa kuzingatia maadili ya Kikristo, viwango vya kitaalamu, na mahitaji ya wakati.

Majukumu ya Idara ya Afya

  • Kusimamia hospitali, vituo vya afya, zahanati, na miradi ya afya chini ya Dayosisi.
  • Kuratibu utekelezaji wa sera na miongozo ya afya kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali na Kanisa.
  • Kuimarisha huduma rafiki kwa jamii kwa kuzingatia afya ya uzazi, watoto, vijana, wazee, na watu wenye mahitaji maalum.
  • Kufuatilia ubora wa huduma za afya, matumizi ya rasilimali, na maendeleo ya watumishi wa afya.
  • Kuwezesha upatikanaji wa huduma za kinga, tiba, marejeo ya rufaa, na elimu ya afya kwa jamii.
  • Kushirikiana na Serikali, mashirika ya kidini, kimataifa na wadau wa afya katika miradi na program za pamoja.

Idara hii inahusisha usimamizi wa taasisi zifuatazo;

  1. Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC)

ALMC ni hospitali ya rufaa ya Kanda, inayotoa huduma za kibingwa na mafunzo kwa wataalamu wa afya. Inahudumia wagonjwa wa ndani na wa rufaa kutoka mikoa mbalimbali.

Huduma: Upasuaji wa moyo na mishipa, huduma ya dharura ya kisasa (emergency medicine), huduma ya macho, fiziotherapia, saratani, ICU, maabara ya kisasa, na huduma za kiroho.

Website: https://almc.or.tz

  1. Hospitali ya Kilutheri Selian

Selian ni hospitali yenye hadhi ya Mkoa, inayotoa huduma za kibingwa kwa jamii ya mijini na vijijini. Imejikita katika huduma rafiki kwa watu wote, hasa maskini na wasiojiweza.

Huduma: Upasuaji, huduma ya mama na mtoto, huduma za maabara, mionzi, , HIV/AIDS, kambi za upasuaji vijijini, n.k.

Website: https://selianlh.or.tz

  1. Vituo vya Afya na Zahanati

Dayosisi inaendesha vituo vya afya na zahanati vijijini kwa ajili ya kuhakikisha huduma zinawafikia watu wa pembezoni. Vituo hivi vinatoa huduma za msingi za afya ikiwa ni pamoja na uchunguzi, tiba, na elimu ya afya. Vituo hivyo ni; Kituo cha Afya Kirurumo, Zahanati 6 ambazo ni Arash, Piyaya, Gelai, Kitumbeine, Ilboru na Kisongo.

Arusha Lutheran Medical Center

Selian Lutheran Hospital

Kirurumo Health Center

Idara ya Hazina

Utangulizi

Idara ya Fedha na Utawala ni nguzo muhimu ya usimamizi wa rasilimali za Dayosisi ya Kaskazini Kati. Lengo kuu la idara hii ni kuhakikisha matumizi ya rasilimali za kifedha, watu, na mali yanazingatia uwajibikaji, uaminifu, ufanisi, na maadili ya Kikristo.

Kwa kushirikiana na vitengo vingine, idara hii inahakikisha kuwa huduma zote za Kiinjili, kijamii na maendeleo zinaendeshwa kwa ufanisi, uwazi, na kwa kuzingatia sheria, taratibu, na kanuni za Kanisa na nchi.

Wajibu wa Idara ya fedha na Utawala:-

  1. Kuandaa, atasimamia na kutekeleza Sera ya Fedha ya Dayosisi
  2. Kaandaa bajeti Jumuishi ya DKAK na Taasisi zake.
  • Kusimamia utaratibu wa manunuzi kwa mujibu wa sheria za nchi na Kanuni za Manunuzi za Kanisa.
  1. Idara inaandaa hesabu ya mapato na matumizi ya mwaka na kuratibisha ukaguzi wa ndani na nje.
  2. Idara inasimamia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

IDARA YA HAZINA

KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI