Idara ya Rasilimali Watu
Idara ya hii inayoshughulikia masuala yanayohusu watumishi wa Dayosisi. Tunaamini kuwa watumishi ni rasilimali muhimu zaidi katika kufanikisha malengo ya Dayosisi yetu. Idara ya Rasilimali Watu inajikita katika kuajiri, kulea, kuboresha, na kuhifadhi vipaji bora vinavyoiwezesha Dayosisi yetu kutoa huduma bora kwa jamii. Miongoni mwa majukumu ya Idara ni pamoja na;
- Kuandaa na kusimamia Sera za utunzaji wa utumishi
- Kuratibu taratibu zote za ajira, tathmini ya utendaji, kupandishwa au kushushwa cheo kwa watumishi, ustawi wa wafanyakazi, motisha, mahitaji ya mafunzo, usitishaji wa ajira na nidhamu.
- Kuhakikisha kuwa kuna uhusiano mzuri katika eneo la kazi na kwamba migogoro yote inatatuliwa kwa wakati kulingana na taratibu za Dayosisi na Sheria za nchi.
- Kuratibu mchakato wa ajira na uajiri wa wafanyakazi wapya.
- Kukuza maendeleo ya kitaaluma kwa wafanyakazi kupitia mafunzo na warsha.
- Kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi na mazingira bora ya kazi.
Dira Yetu:
Kuwa Idara inayoongoza kwa ufanisi, uwajibikaji, na ubunifu katika usimamizi wa rasilimali watu, kwa kuimarisha ustawi na maendeleo ya wafanyakazi kwa ajili ya mafanikio ya taasisi.
Dhima Yetu:
Kutoa huduma bora za rasilimali watu kwa kutumia mifumo ya kisasa, sera bora, na usimamizi wa haki, ili kujenga mazingira ya kazi yenye motisha, heshima, na ufanisi.